Thursday 16 August 2012

Baadhi ya maazimio ya mkutano mkuu wa viongozi

Kufuatia maombi ya wanachama baadhi ya maazimio yaliyofikiwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi uliofanyika Kilimanjaro (Annnual General Meeting) tarehe 27 na 28/07/2012 ni kama ifuatavyo:

1. Kutakuwa na vyeti vya heshima kwa wanachama wote waliotimiza wajibu wao vema katika chama


2. Kuhakikisha Foundation inasajiliwa mapema iwezekanavyo


3. Kuanzia sasa michango yote itakayotolewa kwenye matawi, mwanachama atapewa risiti


4. Ku
tafuta njia nyingine za mapato kama vile uandaaji wa proposal zitakazotolewa kwa mtu yoyote atakayependa kuunga mkono kazi (program) tutakayokuwa tunaifanya

5. Umbwe itakuwa ni eneo rasmi la kuzalishia wanachama wapya wa baadae yaani 'breeding area'

6. Kutoa semina mbalimbali kwaajili ya wanachama kama vile semina za ujasiriamali, za kimasomo n.k

7. Kuanzia sasa fomu za kujiunga zitauzwa kwa Tshs 2,000

8. Taarifa za mapato na matumizi zitatolewa kila baada ya miezi sita

Haya ni baadhi tu yapo mengine pia.

No comments:

Post a Comment