Tuesday 29 January 2013

HAPPY BIRTHDAY UPENDO FOUNDATION!!!


HELLOOOOO!
            UPENDO FOUNDATION inapenda kuwakaribisha wote kujumuika katika siku hii nzuri ya tarehe 29 Januari 2013 kwani leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na inatimiza miaka miwili sasa!!
            Katika kuadhimisha siku hii ya leo ndugu zetu waliopo chuo cha Ushirika (MUCCoBS) walitembelea kituo cha KKKT BCC (Building a Caring Community) kinachotoa elimu kwa watoto wenye ulemavu wa akili kilichopo mkoani Kilimanjaro na kujumuika nao kupata drink and bites lakini pia kutoa msaada uliojumuisha Unga 25kg, Mchele 20kg, Mafuta ya Kupikia lita 10, Chumvi (katoni), Majani ya chai, Sukari 10 kg, Nguo na kadhalika, baadhi ya picha zinaweza kuonekana hapo chini…
            Katika mwaka mmoja uliopita Foundation imefanikiwa kuongeza na kufikia wanachama zaidi ya mia moja (100+) waliopo maeneo mbalimbali haswa vyuoni kama vile MUCCoBS, Mwenge, Mweka, UDSM, IFM, SAUT, MU (Morogoro), MU (Mbeya), IAA, Tumaini Makumira, Tumaini DSM, ARDHI, SMMUCo, UMBWE na kadhalika. Hii ni ishara ya kuendelea kuungwa mkono na wadau walio wengi.
            Mapato ya Foundation kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita yamekuwa ni ya kuridhisha licha ya kwamba majukumu yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa ukilinganisha na vyanzo vya mapato na hii imepelekea Sekretarieti kuja na mipango mbalimbali kwaajili ya kupanua wigo wa mapato lakini pia bado changamoto ni kubwa na hivyo wadau mbalimbali wanakaribishwa kutoa mchango wao wa hali na mali. (taarifa rasmi ya mapato na matumizi itawekwa kwenye mtandao hivi karibuni)
            Kwa mara ya kwanza mwaka uliopita Foundation imeanzisha utararibu wa kutoa semina kwa wanachama wake na hata wale wasio wanachama katika matawi yake kwa kuanza semina juu ya Carrer ilitolewa MUCCoBS na kutokana na mafanikio yake pamoja na kupokelewa vizuri na wanachama basi ni imani yetu semina hizi zitasambaa katika matawi mengine pia.
            Aidha kipindi cha mwaka mmoja uliopita kimeshuhudia kwa mara ya kwanza pia Foundation ikizindua T-shirts! Na hii kazi imeongozwa kwa umakini mkubwa na mafanikio na ndugu zetu waliopo chuo cha Mzumbe tawi la Mbeya, hakika MUNGU awabariki sana. Hivyo basi tunapenda kuchukua furksa hii kuwakaribisheni nyote kununua T-shirts hizo kwaajili yetu, kujenga Foundation yetu na kuitangaza popote pale tutakapokuwepo kwa gharama ya Tshs.10,000 (+gharama za kuisafirisha kama utataka utumiwe nje ya tawi) karibuni sana!!
            Pamoja na hilo mwaka uliopita tumefanikiwa kuendeleza juhudi zetu za kusomesha na kuchangia elimu kwa wanafunzi wenzetu maeneo mbalimbali kadri uwezo ulivyoruhusu. Wanafunzi waliobahatika kupata furksa hii na pamoja na wanafunzi watano kutoka Mwanza, mmoja kutoka chuo cha IFM, mmoja kutoka chuo cha Mzumbe, na wengine watano kutoka shule ya msingi Mzumbe bado tunafanya juhudi kupata takribani tshs. 500,000 fedha taslimu za kuwagharamia elimu yao.
            Hali kadhalika katika mwaka uliopita tumeshuhudia programu kadhaa zikifanyika mkoani Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya na DSM, ni imani yetu program hizi zimeleta tabasamu la ukweli katika maisha ya ndugu zetu.
            Changamoto tulizokumbana nazo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita haswa zimekuwa ni upungufu wa mapato ukilinganisha na mahitaji halisi lakini tunamshukuru MUNGU aliyeinua watu kutoka maeneo mbalimbali kutuunga mkono pale tulipokuwa na uhitaji haswa. Pili, suala la usajili limeendelea kugonga vichwa vyetu kwani mpaka jibu la mwisho tulilolipata ambalo limekuwa changamoto kwetu kupata usajili ni kigezo cha kutakiwa kuwa na Permanent Address kwa maana nyingine ni kutakiwa kuwa na ofisi rasmi, lakini pamoja na hilo juhudi zinaendelea kuona ni namna gani tutalifanikisha hilo. Tatu, ni baadhi ya wanachama na viongozi wa matawi kujisahau kutimiza wajibu wao na hili limepelekea mzigo mkubwa kuangukia Sekretarieti ambayo kimsingi ina majukumu mengi mno ya kitaifa.
            Wito, sekretarieti inapenda kutoa wito kwa wanachama, viongozi wa matawi, wadau mbalimbali na wale wote wanaotutakia heri ndani na nje ya nchi kuendelea kutuunga mkono kwa hali na mali kwani pamoja na kwamba safari tumekwisha ianza ni ukweli usiopingika tunapotaka kufika bado hatujafika lakini MUNGU ametujalia kupata mwanga wa kule tuendako na tunaamini mwaka ujao utakuwa wa mafaniko zaidi kuliko huu uliopita. Tuchukue furksa hii pia kuwaomba wanachama wote kujitahidi kupata T-shirts za Foundation kwaajili ya kujenga Foundation yetu.
            Pia tuwashukuru wale wote walioonyesha ushirikiano wa ajabu katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na hivi sasa Foundation imeanzisha utaratibu wa kuwapatia zawadi ya kutambua michango ya wanachama wake na watu mbalimbali waliojitolea kuifanikisha na kwa kuanza tunaanza na ndugu hawa na tunategemea na wengine watafuata…ndugu, Catherine Anne (SAUT) kwa kuwa tayari kutuunga mkono hata pasipo kuwa na taarifa zetu za kutosha  baada tu ya kututembelea Facebook kwenye page yetu, Vivian Kissela (MUCCoBS) kwa kujitoa kwake kwa hali na mali hata pale ambapo hatukujua cha kufanya yeye alikuja wakati muafaka kutatua changamoto zetu na pia kaka Emmanuel Hosea (UDSM) kwa utayari wake wa kuunga mkono kazi za Foundation pasipo kuchoka, Mmekuwa BARAKA kwetu na MUNGU AWABARIKI SANA!! Na hivyo Foundation inaahidi kuwapatia T-shirts bureeeeeee popote pale mtakapo kuwepo tutawaletea!
            Wengine pia mmekuwa Baraka mno kwetu na ndo maana tunaahidi kuendelea kuwatangaza hapa kadri muda na uwezo unavyoruhusu ila kwa leo tunaomba kuwataja hawa ndugu watatu na kuahidi kuendelea kuwashukuru na wengine.


HAPPY BIRTHDAY UPENDO FOUNDATION!!

Wenu katika kazi
Sekretarieti ya Kudumu




At the BCC Project place...