Sunday 29 January 2012

MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA YA UPENDO FOUNDATION

Tunaadhimisha mwaka mmoja leo hii tarehe 29/01/2012 toka tulipokutana na kuanza rasmi kazi hii mnamo tarehe 29/01/2011 huko Umbwe sekondari tukiwa na wanachama wapatao 30 (wavulana). Tunajivunia mafanikio makubwa tuliyoyapata tangu tulipoanza kuifanya kazi hii ya kujenga jamii yenye tabasamu ( building a smiling society). Miongoni mwa mafanikio tuliyoyapata ni pamoja na kufanya programu tano huko mkoani Kilimanjaro (May), Mwanza (June), Njombe (July), Dar es salaam (August) na Arusha (Septemba). Tumefanikiwa kuyafikia makundi kama vile walemavu, wanafunzi, yatima, wazee, wajane na wengineo, tukitoa msaada wa hali na mali. Mpaka kufikia tarehe 29/01/2012 tulikuwa tumekwisha pokea fedha zifikazo tshs. 687,600 na kutumia fedha zipatazo tshs. 659,100. Hivi sasa tuna wanachama wapatao 90(wavulana kwa wasichana) katika vyuo 12, shule 1, kutoka mikoa 17.
Hivi karibuni tumefanikiwa kutembelea kituo cha watoto yatima cha Rafiki Foundation kilichipo mferejini kimashuku (Kilimanjaro) na kutoa msaada kama vile 25kg mchele, 25kg unga, lita 10 za mafuta ya kupikia, boksi 3 za majani ya chai, 10kg sukari pamoja na katoni moja ya chumvi. Programu hii ilishirikisha wanachama kutoka chuo cha Ushirika (MUCCoBS), chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Umbwe sekondari. Tulikaa nao, tuliwafariji na kuburudika nao!! (Baadhi ya picha zipo hapo chini).
Pamoja na hilo hapo chini kuna taarifa ya mapato na matumizi ya mwka mzima yaani 2011/2012, mwanachama yoyote ambaye atahitaji maelezo ya ziada, kutoa ushauri, maoni, na kadhalika, anaombwa kuwasiliana na viongozi.
MUNGU AWABARIKI NYINYI NYOTE MLIOFANIKISHA HAYA YOTE!!
TUUNGANE KUFIKIA KILELE CHA MAFANIKIO TUYATAKAYO.
“You can have a powerful impact on another human being. The power to preserve another person’s life depends upon your decision. Your generosity and caring can extend life for another person”

PICHA ZA UPENDO FOUNDATION KWENYE PROGRAMU YA JANUARI


Members wa upendo wakiwa na watoto wa Rafiki Foundation














Mtoto wa Rafiki Foundation














Watoto wakiburudika














Tukikabidhi msaada














Wanachama wa Upendo Foundation

No comments:

Post a Comment