Thursday, 16 August 2012

Baadhi ya maazimio ya mkutano mkuu wa viongozi

Kufuatia maombi ya wanachama baadhi ya maazimio yaliyofikiwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi uliofanyika Kilimanjaro (Annnual General Meeting) tarehe 27 na 28/07/2012 ni kama ifuatavyo:

1. Kutakuwa na vyeti vya heshima kwa wanachama wote waliotimiza wajibu wao vema katika chama


2. Kuhakikisha Foundation inasajiliwa mapema iwezekanavyo


3. Kuanzia sasa michango yote itakayotolewa kwenye matawi, mwanachama atapewa risiti


4. Ku
tafuta njia nyingine za mapato kama vile uandaaji wa proposal zitakazotolewa kwa mtu yoyote atakayependa kuunga mkono kazi (program) tutakayokuwa tunaifanya

5. Umbwe itakuwa ni eneo rasmi la kuzalishia wanachama wapya wa baadae yaani 'breeding area'

6. Kutoa semina mbalimbali kwaajili ya wanachama kama vile semina za ujasiriamali, za kimasomo n.k

7. Kuanzia sasa fomu za kujiunga zitauzwa kwa Tshs 2,000

8. Taarifa za mapato na matumizi zitatolewa kila baada ya miezi sita

Haya ni baadhi tu yapo mengine pia.

PICHA ZA DSM PROGRAM

Tuamshukuru MUNGU kwa kufanikisha program yetu ya Dar es Salaam iliyofanyika mwezi Mei na hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa siku hiyo, tunaomba radhi kwa kuchelewa kuwekwa kwenye mtandao kwani ilikuwa juu ya uwezo wetu.. Ikumbukwe wanachama wa DSM walitembelea shule ya watoto wenye ulemavu wa akili iitwayo Sinza Maalum (Sinza Special School)
Asanteni sana! May GOD bless us all

DSM members

Frank and Elisha...
 Pamoja tunaweza!!
 ...getting update about the school

Sinza Special School

It was a happy day for all..