HELLOOOOO!
UPENDO FOUNDATION inapenda
kuwakaribisha wote kujumuika katika siku hii nzuri ya tarehe 29 Januari 2013
kwani leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na inatimiza miaka miwili sasa!!
Katika kuadhimisha siku hii ya leo ndugu zetu
waliopo chuo cha Ushirika (MUCCoBS) walitembelea kituo cha KKKT BCC (Building a Caring Community) kinachotoa elimu kwa watoto
wenye ulemavu wa akili kilichopo mkoani Kilimanjaro na kujumuika nao kupata drink and bites lakini pia kutoa msaada
uliojumuisha Unga 25kg, Mchele 20kg, Mafuta ya Kupikia lita 10, Chumvi
(katoni), Majani ya chai, Sukari 10 kg, Nguo na kadhalika, baadhi ya picha
zinaweza kuonekana hapo chini…
Katika
mwaka mmoja uliopita Foundation imefanikiwa kuongeza na kufikia wanachama zaidi ya mia moja (100+) waliopo
maeneo mbalimbali haswa vyuoni kama vile MUCCoBS, Mwenge, Mweka, UDSM, IFM,
SAUT, MU (Morogoro), MU (Mbeya), IAA, Tumaini Makumira, Tumaini DSM, ARDHI,
SMMUCo, UMBWE na kadhalika. Hii ni ishara ya kuendelea kuungwa mkono na wadau
walio wengi.
Mapato ya Foundation kwa kipindi cha
mwaka mmoja uliopita yamekuwa ni ya kuridhisha licha ya kwamba majukumu
yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa ukilinganisha na vyanzo vya mapato na hii
imepelekea Sekretarieti kuja na mipango mbalimbali kwaajili ya kupanua wigo wa
mapato lakini pia bado changamoto ni kubwa na hivyo wadau mbalimbali
wanakaribishwa kutoa mchango wao wa hali na mali. (taarifa rasmi ya mapato na
matumizi itawekwa kwenye mtandao hivi karibuni)
Kwa mara ya
kwanza mwaka uliopita Foundation imeanzisha utararibu wa kutoa semina kwa wanachama wake na hata wale wasio
wanachama katika matawi yake kwa kuanza semina juu ya Carrer ilitolewa MUCCoBS
na kutokana na mafanikio yake pamoja na kupokelewa vizuri na wanachama basi ni
imani yetu semina hizi zitasambaa katika matawi mengine pia.
Aidha
kipindi cha mwaka mmoja uliopita kimeshuhudia kwa mara ya kwanza pia Foundation ikizindua T-shirts! Na hii
kazi imeongozwa kwa umakini mkubwa na mafanikio na ndugu zetu waliopo chuo cha
Mzumbe tawi la Mbeya, hakika MUNGU awabariki sana. Hivyo basi tunapenda
kuchukua furksa hii kuwakaribisheni nyote kununua T-shirts hizo kwaajili yetu,
kujenga Foundation yetu na kuitangaza popote pale tutakapokuwepo kwa gharama ya
Tshs.10,000 (+gharama za kuisafirisha kama utataka utumiwe nje ya tawi) karibuni
sana!!
Pamoja na
hilo mwaka uliopita tumefanikiwa kuendeleza juhudi zetu za kusomesha na kuchangia elimu kwa wanafunzi wenzetu maeneo
mbalimbali kadri uwezo ulivyoruhusu. Wanafunzi waliobahatika kupata furksa hii
na pamoja na wanafunzi watano kutoka Mwanza, mmoja kutoka chuo cha IFM, mmoja
kutoka chuo cha Mzumbe, na wengine watano kutoka shule ya msingi Mzumbe bado
tunafanya juhudi kupata takribani tshs. 500,000 fedha taslimu za kuwagharamia
elimu yao.
Hali
kadhalika katika mwaka uliopita tumeshuhudia programu kadhaa zikifanyika mkoani Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya na
DSM, ni imani yetu program hizi zimeleta tabasamu la ukweli katika maisha ya
ndugu zetu.
Changamoto tulizokumbana nazo katika
kipindi cha mwaka mmoja uliopita haswa zimekuwa ni upungufu wa mapato
ukilinganisha na mahitaji halisi lakini tunamshukuru MUNGU aliyeinua watu
kutoka maeneo mbalimbali kutuunga mkono pale tulipokuwa na uhitaji haswa. Pili,
suala la usajili limeendelea kugonga vichwa vyetu kwani mpaka jibu la mwisho
tulilolipata ambalo limekuwa changamoto kwetu kupata usajili ni kigezo cha
kutakiwa kuwa na Permanent Address
kwa maana nyingine ni kutakiwa kuwa na ofisi rasmi, lakini pamoja na hilo
juhudi zinaendelea kuona ni namna gani tutalifanikisha hilo. Tatu, ni baadhi ya
wanachama na viongozi wa matawi kujisahau kutimiza wajibu wao na hili
limepelekea mzigo mkubwa kuangukia Sekretarieti ambayo kimsingi ina majukumu
mengi mno ya kitaifa.
Wito, sekretarieti inapenda kutoa wito
kwa wanachama, viongozi wa matawi, wadau mbalimbali na wale wote wanaotutakia
heri ndani na nje ya nchi kuendelea kutuunga mkono kwa hali na mali kwani
pamoja na kwamba safari tumekwisha ianza ni ukweli usiopingika tunapotaka
kufika bado hatujafika lakini MUNGU ametujalia kupata mwanga wa kule tuendako
na tunaamini mwaka ujao utakuwa wa mafaniko zaidi kuliko huu uliopita. Tuchukue
furksa hii pia kuwaomba wanachama wote kujitahidi kupata T-shirts za Foundation
kwaajili ya kujenga Foundation yetu.
Pia
tuwashukuru wale wote walioonyesha ushirikiano wa ajabu katika kipindi cha
mwaka mmoja uliopita na hivi sasa Foundation imeanzisha utaratibu wa kuwapatia
zawadi ya kutambua michango ya wanachama wake na watu mbalimbali waliojitolea
kuifanikisha na kwa kuanza tunaanza na ndugu hawa na tunategemea na wengine
watafuata…ndugu, Catherine Anne (SAUT)
kwa kuwa tayari kutuunga mkono hata pasipo kuwa na taarifa zetu za kutosha baada tu ya kututembelea Facebook kwenye page
yetu, Vivian Kissela (MUCCoBS) kwa
kujitoa kwake kwa hali na mali hata pale ambapo hatukujua cha kufanya yeye
alikuja wakati muafaka kutatua changamoto zetu na pia kaka Emmanuel Hosea (UDSM) kwa utayari wake wa kuunga mkono kazi za
Foundation pasipo kuchoka, Mmekuwa BARAKA kwetu na MUNGU AWABARIKI SANA!! Na
hivyo Foundation inaahidi kuwapatia
T-shirts bureeeeeee popote pale mtakapo kuwepo tutawaletea!
Wengine pia
mmekuwa Baraka mno kwetu na ndo maana tunaahidi kuendelea kuwatangaza hapa kadri muda na
uwezo unavyoruhusu ila kwa leo tunaomba kuwataja hawa ndugu watatu na kuahidi
kuendelea kuwashukuru na wengine.
HAPPY BIRTHDAY UPENDO FOUNDATION!!
Wenu katika kazi
Sekretarieti ya Kudumu
At the BCC Project place...